World Bank Visit

IMG_5410-minJPGTimu ya wasimamizi wa mradi wa LVEMP II kutoka benki ya Dunia watembelea mradi kufuatilia utekelezaji washughuli za kupunguza uchafuzi wa Mazingira ya Ziwa Victoria.
Timu hiyo ya wataalamu ikiongozwa Bwana Jian Xie ambaye ndie msimamizi wa LVEMP II ndani ya Benki, imetembelea miradi inayotekeleza katika Halmashauri ya Maswa, Ilemela na Nyamagana.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ukarabati wa machinjio ya Jiji la Mwanza yenye mfumo wa kutibu maji taka, ujenzi wa vyoo katika shule ya Isenga, udhibiti na uopoaji wa gugumaji, uunganishwa wa kaya katika mufumoa wamaji taka katika kata za Kirumba na Kirangiri, udhibiti na uopoaji wa gugumaji na ujenzi wa maabara ya ubora wa maji Mwanza.
Miradi mingingine ni uhifadhi wa dakio la Mto Simiyu wilayani Maswa katika kijiji cha Malita kwa njia ya ufugaji nyuki na upandaji wa miti ndani mita sitini (60) ya mto, visima vya maji kwa matumiza ya binadamu na mifugo, ufugaji wa ng’ombe wa kisasa wa maziwa, matumizi ya biogasi inayotokana na kinyesi cha wanyama na majiko banifu na sanifu.
Miradi hii yote kwa pamoja inalenga kupunguza uharibifu na uchafuzi wa mazingira ya Ziwa Victoria unaosabaishwa na shughuli za kibinadamu zisizo rafiki na endelevu kwa mazingira.