Ziara ya Kamati ya taifa ya Uchumi ya Uganda

1-minJPGKamati ya Bunge la Uganda inayoshughulikia mambo ya Uchumi, imefanya ziara ya siku 3 katika miradi inayotekelezwa na LVEMP II katika miji ya Bukoba na Mwanza. kwa upande wa Bukoba Manispaa kamati ilitembelea Mfumo wa Kutibu Majitaka uliopo eneo la Nyanga baada ya kusalimana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawiro. Mhe. Kinawiro aliwakaribisha Waheshimiwa Wabunge hao katika mkoa na nchini. Aidha kamati pia ilitembelea Ukarabati wa Machinjio katika jiji la Mwanza ambayo imeunganishwa na mfumo wa kutibu majitaka sambamba na mtambo wa kutengeneza gesi inayotokana na kinyesi cha ng’ombe ambapo gesi hiyo itatumika katika kuendesha shughuli katika machinjio. Vilevile Kamati iliona eneo lililotolewa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Uokozi na Uratibu katika Ziwa Victoria ambapo Makao Makuu yatakuwa Mkoani Mwanza ( Tanzania) na vituo vingine viwili katika miji ya Kisumu na Entebbe(Uganda) kwa ajili ya kupunguza vifo visivyo vya lazima.